• sl-7.png
  • sl-5.png
  • sl-6.png
  • sl-4.jpg
  • sl-3.jpg
  • sl-2.jpg
  • sl-1.jpg

Unpublished

Sinodi (Bunge) Maalumu ya Kanisa la Anglikana Tanzania, ilivyo kaa kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa Anglikana Tanzania, leo tarehe 15 Februari, 2018 imemchagua Askofu Maimbo Mndolwa kuwa Askofu Mkuu wa Saba wa Kanisa Anglikana Tanzania akimfuatia Askofu Mkuu wa sasa anaye maliza muda wake Dr.Jacob Erasto Chimeledya.

Askofu Mndolwa ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga na aliitwa kwenye huduma ya Mungu katika Daraja Takatifu la Uaskofu tarehe ya Nne ya Mwezi wa Tisa katika mwaka wa Bwana wetu Yesu Kristo wa Elfu Mbili na Kumi na Mbili.

Askofu Mkuu Mteule amewaeleza wajumbe wasinodi, Kanisa la Anglikana Tanzania na duniani, pamoja na umma wote kwamba amepokea kwa unyeyekevu nafasi hii na kuahidi kutumikia jamii na kanisa kwa moyo wake wote. Akitoa Baraka za mwisho baada ya kumalizika kwa utaratibu wa kumchagua, Askofu Mkuu Mteule amesisitiza amani, mshikamano na kumsikiliza Mungu katika maisha yetu. Askofu Mndolwa kama Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa Anglikana Tanzania, atasimikwa katika Ibada Takatifu tarehe 20 May 2018 siku ya Bwana ya Pentekoste. Imetolewa nasi, kwa Neema ya Mungu:

ALMANAC

Login